Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na kuzama kwa Meli ya Star Gate hukokatika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.
Wananchi mbalimbali wakishuhudia tukio la kuokolewa watu waliozama na meli ya Star Gate huko katika hukokatika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akiwa katika Eneo la Bandari akishuhudia kuletwa kwa majeruhi mbalimbali waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Amer Kificho pamoja na mawaziri mbalimbali wakiwa katika Eneo la Bandari wakishuhudia kuletwa kwa majeruhi mbalimbali waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Askari wa Vikosi mbalimbali wakiwa katika kazi ya Uokozi kwa Abiria waliokuwa katika Meli ya Star Gate ambayo iliozama katika ikiwa imebeba abiria 250 huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar.
Majeruhi alieokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.
Majeruhi wakipatiwa Mablangeti kwa ajili ya kujihifadhi baada ya kuokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.


BOFYA HAPA KUONA PICHA ZINGINE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2012

    Poleni sana ndugu zetu mliokuwa mbali na sisi,Mnyeezi Mungu awalinde wote muokolewe salama inshallah!Yarabi Salama!

    ReplyDelete
  2. Namkeleja HJuly 19, 2012

    tutandelea mpaka lini kuona maisha ya watanzania na wasio watanzania wanaosafiri na Tanzania yakiwa hatarini pale wanapokuwa safarini. Ajari halisi haziepukiki ila kuna uwezekano wa kuepusha ajali zinazotokana na mapungufu ya kiutendaji katika ngazi mbalimbali katika sekta ya uchukuzi. Polen kwa wasafiri, ndugu jamaa na watanzania wote kwa ajali hii ya meli ambayo inatukumbusha machungu ya ajali ya Mv spicelanders. hongera kwa vyombo vya usalama, serikali watu binafsi na mashirika kwa kushirikiana kuokoa maisha ya viumbe hawa wasiokua na hatia.
    Wito wangu ni kwamba ingawa hatujui chanzo cha kuzama kwa meli hii wote kwa nafasi zetu yaan serikali wamiliki wa vyombo vya uchukuzi, abiria, vyombo vya usalama na wadau wote wa sekta ya uchukuzi na usafirshaji ni wakati muafaka sasa kwanza kuwa na mkakati na kutekeleza mkakati wa kupunguza ajali zinazotokana na uzembe fulan, pili kuwa tayari wakati wote kukabiliana na majanga hasa uokoaji tuimalishe miundombinu ya uokoaji (vifaa, watu, na uharaka wa kufika maeneo ya tukio, tatu usimamizi thabiti wa sheria zetu ( maisha ya watu yawe mbele kuliko maslahi binfsi ambayo mara nyingi yamekuwa yakisababisha kukiukwa kwa sheria) nne kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri wanafilosophi wanakinzana kwamaba i "every money is enough" wengine wanasema "no money is enough" mi nakubaliana na na wakwanza kwmba every money is enough kwahiyo wamiliki wa vyombo vya usafiri wachukue hiyo slogan kwa kuweka maisha ya watu mbele bila kujali kiasi cha fedha watakosa. Seketa ya usafirishaji ni muhimili muhimu kwa maendeleo ya yeyote duniani kwahiyo lazima iimarishwe si tu kwa kujenga barabara na bandari nzuri kwa upande serikali lakini kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri lazima wazingatie ubora wa vyombo hivo pia kwa wasimizi wa sheria lazima wajinge vizuri. Tukiyapuuza haya mustakabali wa taifa letu sio nzuri tutaendelea kupoteza nguvu kazi ya taifa, hofu zitatujaa watanzania na maendeleo itakua ni ndoto kwetu.
    Ahsante sana

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 19, 2012

    Poleni sana.Mdau yeyote anayefahamu boat kwa kiswahili inaitwaje?(boti?).Meli(Ship?).Boat/ship nadhani ni vyombo vinavyoelea majini,kubeba abiria na mizigo, tofauti nadhani ni Ukubwa wa chombo.Vyombo vingi vya habari vimeripoti MELI imezama..Kwa Watanzania wanaoishi kando ya ziwa Victoria ukitaja meli tu akili inakimbilia chombo kikubwa cha majini kama M.V Victoria.BAKITA saidia hapa..."Meli ndogo yazama..."?

    David V

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 19, 2012

    poleni sana wahanga wote na waliopoteza ndugu na marafiki ,Mungu awaweke mahali salama................TUNAHITAJI KUJIPANGA (PREPAREDNESS ) kwenye majanga ,tungekuwa tunajipanga vizuri tungeokoa maisha ya watu wengi!

    ReplyDelete
  5. Poleni sana nyote mliofikwa na ajali hii na waliopoteza maisha yao, MWENYEEZ MUNGU UWAGHUFIRIE KWA YOTE NA UWALAZE PEMA PEPONI - AMEN.

    Hivi ni kweli lakini chombo hicho kilikuwa kimepakia hao abiria 250 tu au tena yasijekuwa kama yale yale ya M.V.Spice. Kudai idadi kadhaa kumbe ilikuwa imepakia kufurutu ada. Poleni sana ndugu zangu wa Visiwani, machungu ya SPICE bado tungali nayo, mengine haya mapya yametufika. INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIUN.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 19, 2012

    ushauri wangu ni bora ijengwe barabara kutoka zanzibar mpaka Dar na pemba mpaka unguja bila hivyo hili tatizo halitokwisha maisha!! kama tunavyoona wenyewe vyombo vinazama ovyo.

    ReplyDelete
  7. MsemaKweliJuly 19, 2012

    Hivi regulation za mambo ya usafiri wa maji Tanzania upoje? Boti hazitakiwi kuwa na lifesaving jackets?

    Halafu nasikia hali ya hewa ilikuwa mbaya sana (upepo mkali) Je, safari zote za boat hazitakiwi kuzingatia hali ya hewa kabla ya kuanza safari?

    Taarifa inasema kuwa boat ilikuwa na watu 200 lakini taarifa ingine inasema watu 400. Je taarifa sahihi ni ipi?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 19, 2012

    Namkeleja H, katika majanga kama haya , ndugu zanguni tuweni na subira,siyo pupa na kuanza kutaja mambo ambayo hayajajulikana bado, sasa ,aa !!! mara money is not enough,mara maendeleo itakuwa ndoto, haya yote yamekuja baada ya ajali ?? vyombo vya usafiri vizibitiwe ,siyo kujenga mabarabara tu na bandari pia !! haya yote yanahusu nini na ajali hii ?? inaonekana wewe ndugu ,kama ungelikuwa hakimu,basi taifa zima lingeishia segerea. Please dont judge. Vuta subira,uchunguzi utafanyika. Pia elewa kwamba katika maisha ,dhoruba na misukosuko kama hii LAZIMA itakuwepo tu. pande zote za dunia, leo utasikia ,Phillipines nako meli imezama, au ndege imeanguka au treni zimegongana huko India nakadhalika,haipiti mwezi ,utasikia jambo. Tupo duniani,majanga kama haya hayataepukika, tuacheni tabia za kushutumu bali tujengeni moyo wa kukubali matokeo. Kwani jamani ,swali la kizushi, KWANI bahari kuchafuka ,hili nikosa la mfanyabiashara wa hiyo meli ?? Na wewe David, jina Meli ni sahihi kabisa kutumika, inaweza kuwa meli kubwa au meli ndogo,inaweza kuwa meli ya abiria au meli ya mizigo, sasa hao watu wanaoishi ziwa victoria ,cha kuwashitua hapa ni nini ?? muonekano wa hicho chombo kilichozama ni wa meli,siyo pantoni,wala mtumbwi. Nitafurahi kusikia kama mchango wangu wa mawazo umesaidia.Asanteni.Zebedayo

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 19, 2012

    Why this has happened again after MV Spice Islander just last year in Sept 2011. If the weather was bad, they would have not let any vessels leave the ports at all on 18th July, in other countries flights get cancelled due to BAD WEATHER lakini here it is Bahati Mbaya after live are lost.
    What is this Govt up to?... From Nungwi to Stone Town you see 5 to 6 traffic stops, for no reason, does this apply in the Boats, when the vessel is overly filled with people and cargo, is there someone checking ama ni Bahati Mbaya baada ya ajali kutokea.

    A very bitter citizen of TZ

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 19, 2012

    I feel sad for the lives lost of innocent people. What happens if Port Authority declare as a bad weather and stop all the vessels from leaving the ports in DAR and ZNZ. Lives would be saved, lakini after the ajali kutokea, we blame it on the weather, did nobody check the weather before kupakia watu on the boat?
    Our friends in other countries cancel flights due to bad weather, we should do the same. From Nungwi to Stone Town, you get stopped for 5 to 6 times by police who waste your time for no reason, kwanini nobody was there to check at the Port, wakati MV Spice Islander sinked in Sept 2011, they should have been extra careful and learnt from the mistake!
    Jamani, Tanzania wake up and raise questions as the big guys dont get affected, they travel on planes, it is the small people who use the boats!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...